Nifanyeje nikishika mimba ambayo sikuipangia

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nifanyeje_nikishika_mimba_ambayo_sikuipangia

Click Code to Download

Huenda umeshika mimba ikiwa umeshiriki ngono na hedhi yako imechelewa, unahisi uchungu kwenye matiti, unaenda haja ndogo mara kwa mara na unahisi kutapika. Muone mhudumu wa afya au mkunga haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa wewe ni mja mzito.

Wasichana wengi hushika mimba bila wao kutarajia. Baadhi yao hupata usaidizi kutoka kwa familia na marafiki wao. Kwa wengine, mambo sio rahisi.

Ikiwa unataka kuavyaa mimba kwa sababu unaona imekunfunga, tahadhari sana na uamuzi wako. Zungumza na mtu mzima unayemuamini. Maisha yako ni ya muhimu sana kupotea. Duniani kote, wanawake na wasichan hupoteza maisha yao wakijaribu kuavyaa mimba kutumia njia ambazo hazifai. Kuna njia salama za kuavyaa mimba.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020819