Nitajuaje ikiwa niko katika hatari ya ugonjwa wa zinaa

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nitajuaje_ikiwa_niko_katika_hatari_ya_ugonjwa_wa_zinaa

Click Code to Download

Baadhi ya wanawake, na hata wanaume, ambao wameambukizwa na magonjwa ya zinaa, hawana ishara zozote.

Hata kama hauna ishara zozote, uko katika hatari ya ugonjwa wa zinaa ikiwa:

  • mpenzi wako ana ishara za ugonjwa wa zinaa. Huenda amekuambukiza, hata kama hauna ishara.
  • una zaidi ya mpenzi mmoja. Unapokuwa na wapenzi wengi, huenda mmoja wao amekuambukiza ugonjwa wa zinaa.
  • umekuwa na mpenzi mpya katika miezi 3 iliyopita. Huenad alikuwa na mpenzi mwingine kabla ya wewe, ambaye alikuwa na ugonjwa wa zinaa.
  • unafikiri kuwa mpenzi wako ana wapenzi wengine (kwa mfano, ikiwa anaishi mbali na nyumbani). Hii inamaanisha kuwa ni rahisi kwake kuambukizwa ugonjwa wa zinaa, na kukuambukiza pia.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010506