Nitawezaje kuzuia ndoa ya kulazimishwa au kupelekwa kufanya kazi

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nitawezaje_kuzuia_ndoa_ya_kulazimishwa_au_kupelekwa_kufanya_kazi

Click Code to Download

Wakati mwingine, familia itamuoza msichana mdogo kwa mwanaume mzee ili kulipia familia deni. Wanaweza pia kumuuza ili wapate pesa au kitu kingine ambacho familia inahitaji.

Wakati mwingine wasichana hawa hupelekwa mji au jiji lingine. Wao hufikiri kuwa wanaenda kufanya kazi kwenye viwanda, au kuwa yaya, lakini wao hulazimishwa kushiriki ngono kwa malipo.

Ikiwa unafikiri kuwa wewe au msichana mwingine katika jamii yako analazimishwa kuolewa, au kupelekwa kufanya kazi, tafuta usaidizi kutoka kwa mtu unayemuwamini. Mtu huyo anaweza kuwa mjomba au shangazi, au mwalimu wako wa kike.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020818