Nitamshawishi vipi mpenzi wangu kutumia komndomu

Kutoka Audiopedia Swahili
Pitio kulingana na tarehe 14:51, 17 Februari 2022 na Audiopedia Admin (Majadiliano | michango) (XML import)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nitamshawishi_vipi_mpenzi_wangu_kutumia_komndomu

Click Code to Download

Utumizi wa kondomu ni njia mojawapo rahisi sana ya kuzuiamaambukizi na mimba zisizotakikana. Lakini, sio watu wengi huzitumia mara ya kwanza. Hapa kuna malalamishi kuhusu utumizi wa kondomu:

"Nilizitumia mara ya kwanza na sikuzipenda." Inachukua muda kuzoea kutumia kondomu. Kubalianeni kuwa mtazitumia kwa wiki kadhaa. Mara nyingi, wapendanao watagundua kuwa wanafurahia ngono kama hapo awali, wakitumia kondomu.

"Sihisi chochote ninapovalia kondomu." Tumia mafuta kama vile K-Y jelly. Mafuta haya hufanya ngono kuwa nzuri kwa wapenzi wote wawili. Weka tone moja la mafuta haya kwenye ncha ya kondomu kabla ya kuivaa. Ni kweli kuwa ngono ni tofauti unapotumia kondomu. Hata hivyo, watu wengi wanakubaliana kuwa, heri kushiriki ngono ukiwa umevalia ondomu kuliko kukosa kuivalia kondomu kabisa! Kondomu pia huwasaidia baadhi ya wanaume wakiwa wamesisimka kwa mda.

"Hatujawahi kutumia kondomu. Mbona tuanze sasa?" Elezea kuwa sasa unaelewa hatari za kushiriki ngono ambayo sio salama, na ni jambo jema mkijilinda. Unaweza kumpa sababu kama vile, ungependa kubadilisha njia ya kupanga uzazi.

"Sipendi kuacha ninachofanya ili kuvaa kondomu." WEka akiba ya kondomu mahali ambapo mnapenda kushiriki ngono ili usianze kuzitafuta baadaye. Mara uume wake unaposisimka, mwanaume anaweza kuvaa kondomu, kisha muendelee na shughuli yenyu. Ikiwa kondomu za kike zinapatikana na unaweza kuzigharamia, unaweza kuzitumia pia, ambazo huvaliwa mbeleni.

"Siwezi kugharamia kondomu, aukondomu hazipatikani." Vituo vingi vya afya, na mashirika ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI hupeana kondomu bure au kwa malipo duni sana. Ingawaje unaweza kurudia kutumia kondomu kuliko kukosa kutumia kondomu, ni vyema ukitumia kondomu mpya kila wakati. Ikiwa ni lazima urudie kutumia kondomu, ni vyema ukiziosha kwa maji na sabuni, kisha uzianike vyema zikauke, kisha uzikunje namna zilivyokuwa zimekunjwa awali na uziweke mahali pasipo na joto. Tumia njia zingine kupunguza hatari. Kwa mfano, ni salama kwa mwanaume na mwanamke ikiwa mwanaume ataondo auume wake kabla hajamwaga mbegu. Ikiwa ni shida kupata kondomu, basi unaweza kutumia karatasi ya plastiki.

"Sihisi uhusiano". Jaribu kufanya utumizi wa kondomu kuwa jambo la kufurahisha. Fanya mazoezi ya jinsi tofauti za kuvaa kondomu, kisha uifanye kama mchezo mdogo kabla ya kushiriki ngono. Mnaweza kuwacha kutumia kondomu siku za usoni, ikiwa unamwamini mpenzi wako, na kuna huduma za uchunguzi wa virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa karibu. Ni vyema nyote mkipmwa, muendelee kutumia kondomu kwa miezi 6, kisha mkapimwe tena. Zungumzeni kuhusu umuhimu wa kuwa salama, uaminifu na utumizi wa kondomu kila mara, ikiwa mmoja wenyu atashiriki ngono na mtu tofauti.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010512